
Virusi vya korona si za kawaida; watu tofauti huathirika kwa njia tofauti. Virusi hivi husababisha kukohoa, joto ya mwili ama kuathirika kwa uwezo wa kupumua na kuonja. Wengine, hupata shida za tumbo, kuendesha na upele wa Ngozi.
Watu wengi, hawaonyeshi dailili za viursi vya Korona, lakini wanaweza kusambaza kwa watu wengine (wao ni 'asymptomatic'). Hii ndio sababu, Korona inasambaa kwa urahisi.
Ikikithiri, Korona inaweza kuleta shida za kupumua, kushindwa kwa viungo vya mwili, ambayo mwisho wake ni kifo. Wazee na wamama wajawazito wako katika hali hatari Zaidi ya kufariki kutokana na virusi hivi.
Watoto pia wanaweza kuambukizwa virusi hivi vya Korona, lakini ni vigumu wawe wagonjwa kama watu wazima. Watoto wengi hawaonyeshi dalili za virusi hivi, ndio maana shule zimekuwa njia moja wapo kuu ya kusambaza virusi hivi.
Kuna watu ambao huonyesha dalili za kukaa kwa muda, lakini hii inahitaji utafiti Zaidi. Wengi wameripoti kuwa na shida za kupumua, udhaifu wa misuli, afya ya kiakili na dalili nyingine.