
Kuna wale ambao walikuwa na virusi vya Korona, hata kama walienda hospitalini, bado wanazidi kupata dalili za korona baada ya miezi. Hii inaitwa Korona Ya Muda.
Shida hizi ni kama:
- Msongo wa mawazo
- Shida na kupumua
- Kuchanganyikiwa na kusahau
- Udhaifu wa misuli
- Shida za tumbo
- Uchovu wa kimwili.
Wazee na wanaume wako kwa hatari Zaidi ya kuwa na shida za kupumua na shida za kiakili. Vijana na wanawake wako katika hatari Zaidi ya kuumwa na kichwa na kuwa na msongo wa mawazo
Dalili hizi na vinavyovisababisha bado hazielweki vizuri. Kama wewe ama mtu unayejua anashida, ni vizuri kutafuta ushauri kwa mhudumu wa afya.