Chanjo ya Korona

Chanjo hizi zinatayarisha mwili wako kwa maambukizi yajayo.

Kama Chanjo nyingine, hizi haziwezi kutibu Korona. Lazima upate chanjo kabla hujaambukizwa na virusi ya Korona.

Chanjo hizi hutayarisha mfumo wako wa kinga. Zinasaidia mwili wako kujenga kinga ya kuweza kutambua na kupinga virusi vya korona, kama utaambukizwa.

Wengi hupata chanjo mbili dhidi ya korona, ya pili ukiipata baada ya miezi kadhaa baada ya kupata ya kwanza.

Kuna athari ndogo za kimwili zinazoweza kuja na chanjo hizi(uchungu mwilini, kuumwa na kichwa, joto ya mwili) ambayo ni kawaida. Hii ni ishara nzuri ya kwamba mfumo wako wa kinga unajitayarisha kupingana na virusi vya Korona.

Baada ya kupata chanjo, unashawishiwa uzidi kuvaa barakoa wakati uko mahali kuna watu wengi. Unashawishiwa pia uepukane kutengamana na watu wengi. Bado unaeza kupata Korona hata kama umepata chanjo. Chanjo hii hukusaidia kupingana na mabaya ya virusi vya Korona, lakini bado unaweza kusambaza virusi hivi kwa watu wengine, hata kwa wale ambao wako karibu na wewe.