
Ujauzito
Wanawake wajawazito wako katika hatari Zaidi kutokana na virusi vya korona, inayoweza kusababisha kifo. Pia inaongeza uwezo wa kupata mtoto kabla muda, au kuzaa mtoto kama amefariki dunia.
Ingawa kulikuwa na hali ya tahadhari kuhusu chanjo kwa wanawake wajawazito, kwa sasa tunajua kwao, chanjo ni salama, kuwasaidia kuwalinda kutokana na magonjwa mabaya. Milioni ya wanawake tayari washapata chanjo. Hakikisha umeoata ushauri kutoka kwa daktarin wako kama uko na hali nyingine za kiafya na unaeza kuwa kwa hali hatari kwa sababu moja ama nyingine.
Kunyonyesha
Kama uko na virusi vya Korona na unanyonyesha, ni afadhali uvae barakoa na kuosha mkono, kulinda mtoto wako asiathirike.
Hakuna sababu zozote za kiafya za kupinga kuchanjwa kwa wanawake wanaonyonyesha.