Vikundi Vilivyo Kwa Hatari

Kuna walio katika hatari Zaidi ya kupata virusi vya Korona, nao ni:

  • Watu walio na umri unaozidi 65
  • Walio na saratani
  • Walio na ugonjwa ya kisukari
  • Walio wanono kupita kiasi
  • Wajawazito
  • Walio na ugonjwa wa moyo au mapafu
  • Walio na mfumo dhaifu wa kinga

Panapofaa, vikundi hivi vinafaa kupewa kipao mbele kupata chanjo. Wanafaa pia kuzidi kuvaa barakoa na kuepekuna kutengamana na watu ambao wanakisiwa kuwa na virusi.

Wanaofanya kazi na watu wengi, kama vile wafanyikazi wa kiafya, pia wako kwa hatari Zaidi ya kupata virusi hivi. Wanafaa kupewa kipao mbele kupata chanjo, kujilinda wenyewe na kusimamisha kusambaza kwa virusi ya Korona kwa vikundi vilivyo kwa hatari.