Jinsi ya Kujikinga

Korona husambaa haswa kupitia hewa kutoka kwa wale ambao wameambukizwa na virusi hivi. Virusi hivi husambaa hewani na huweza kubaki hewani kwa muda kama vile moshi wa sigara.

Barakoa, hewa safi na umbali wa kimwili zinaweza kukusaidia kujikinga na virusi hivi. Kuosha mkono muda baada ya nyingine na kutumia sanitaiza kila wakati pia ni njia mwafaka za kujikinga na virusi hivi.

Epuka kujumuika kwenye maeneo ya ndani ya wenye watu wengi kama vile baa, klabu, msikiti na Kanisa.

Kupata chanjo dhidi ya Korona haizui kupata Korona ama kuambukiza wengine, lakini inapunguza hatari ya kuwa na magonjwa mabaya.

Wakati umechanjwa, zidi kuchukua tahadhari na kuvaa barakoa.