
Kuna uvumi mwingi unasambazwa kuhusu janga la Korona.
Hii ndio ukweli:
- Korona ni hatari, imeuwa Zaidi ya watu milioni 10
- Chanjo ni salama, zimesaidia kuwakinga mamilioni ya watu.
Ni kawaida kuwa na uoga kuhusu Korona. Janga hili limetenga watu na kuwalazimisha kugeuza tabia zao. Nayo pia imeleta shida nyingi za kifedha.
Ni vigumu sana kubaki umeogopa virusi ambavyo hatuoni na macho, kibinadamu, tunabaki kuweka lawama kwa vitu tunavyokisia. Hii ndio kwa maana kuna uvumi mwingi umeenezwa kuhusu ugonjwa huu.
Nchini Kenya, uvumi ulienezwa kwa sababu hatukuona watu wengi wakiathirika na ugonjwa huu. Wengine wakaeneza uvumi wakiamini wanasaidia wengine. Wakati mtu anaaza kuamini uvumi huu, ni vigumu sana kumrudisha na kumweleza ukweli. Wanahitaji ukweli usiotingisika kutoka kwa watu ambao wanaamini.
Watu wengi wameathirika na Korona, lakini sasa tuko na Chanjo za kutusaidia kupigana nayo. Tunaamini ya kwamba watu wengi wanaweza kupata chanjo kama watapata Habari inayaofaa.